Pages


Saturday, June 30, 2012

KWA WAKAZI WA ARUSHA NA VITONGOJI VYAKE MMESIKIA HII? FUATILIA MAANA SI YA KUKOSA HII...!


Mahali ni pale pale Club AQ,njoo uone vijana waliofika fainali wakiwania nafasi ya kurekodiwa audio na video huku ukipata burudani safi toka kwa wazee wa kulalisha Jambo Squad,ni kuanzia saa 4 usiku,jumamosi hii kwa kiingilio cha Tsh5000 tu,,,
Rap Race imedhaminiwa na Grandmaster Productions,Sosh Graphix,Triple A fm,Radio 5,Sibuka fm,Tv Sibuka,Club AQ na Helping Hands

Sunday, June 24, 2012

PICHA 9 ZA MISS ARUSHA- WARIDI FRANK NDIO MISS ARUSHA 2012!

Diamond Akitoa Burudani  katika Mashindano hayo

Diamond Juu Ya Jukwaa la Mamiss

MISS ARUSHA 2012 WARID FRANK

MISS ARUSHA NA 1 WARID FRANK KATIKA VAZI LA UBUNIFU

 MISS ARUSHA NA 2 SARAH BENJAMIN KATIKA VAZI LA UBUNIFU

MSANII SAM WA UKWELI AKITO BURUDANI

 MISS ARUSHA TANO BORA

 MISS ARUSHA NA 3 ANITHA BENJAMIN KATIKA VAZI LA UBUNIFU

MASHINDANO YA KUMTAFUTA MREMBO WA JIJI LA ARUSHA MISS REDDS ARUSHA 2012 YAMEFANYIKA JIJI HAPA KATIKA HOTELI YA MOUNT MERU HUKU MREMBO WARID FRANK AKIIBUKA MSHINDI, NAMBA 2 IKISHIKWA NA SARAH BENJAMIN NA ANITHA SEBASTIAN AKISHIKA NAFASI YA TATU.

PICHA ZOTE NA DJ NASS

Friday, June 22, 2012

DOGO JANJA ATUA DAR KAMA MFLAME NA HIVI NDIVYO ALIVYO POKELEWA










 Dogo Janja ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi na kusisitiza kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho amekikubali kwa roho safi.

Janja amesema bado hajasaini mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu wake wawili anaowasubiri kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba, baada ya hapo ndio atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza.

Amesema amebadili mawazo na sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri ambayo aliahidiwa na Ostaz Juma meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa shule na kurudishwa nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni kusoma kwenye shule binafsi nzuri na pia swala lake la muziki kuzingatiwa.

kwenye sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati”
Kwa kumalizia Janja amesema kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli mbiu ya wakati nilivyokujaga nilisema nawakalisha matembo sasa hivi nawalaza chali matembo”

Tuesday, June 19, 2012

Madee WANTED (Arachunga) Arusha!





Kama kawaida yao kwa machalii wa Arusha (A-Town) ni kwamba ukimzingua chalii mmoja wa Arachuga tambua kuwa umemess up na mji mzima.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika toka A-TOWN ni kwamba kama Madee asipoonyosha maelezo yake kuhusu haki ya Dogo Janja ama kuomba radhi kwa walichomfanyia (Tip Top Connection), Arusha itakua chungu kwao. Kuna wale wanaosema kuwa wakimwona Arusha basi atarudi Dar jina tu.

Wapenzi wa hip hop jijini Arusha wana hasira na Madee kwakuwa wanaamini kuwa amemdhulumu Dogo Janja haki yake na kama asipoenda hewani kukiri kosa lake mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwake.

HUU NDIO MKOKO WA DIAMOND KITU CHA MILIONI 60

Staa wa muziki wa kizazi kipya  Bongo, Naseeb Abdul  ‘Diamond  Platinumz’ amevuta mkoko wa Kijanja  wenye thamani ya ‘mkwanja wa Kibongo Milioni  60 keshi.


“Nashukuru Mungu kuwa mpango wangu umetimia, nilipanga hivi kitambo lakini kuna baadhi ya mambo yalichelewesha hatua hiyo, najua watu watasenama mengi kuhusu hili lakini ukweli ni kuwa huu ni mchuma wangu” alisema Diamond.




Katika hatua nyingine Diamond alifunguka kuwa awali alinunua mdinga kama hiyo huko visiwani Zanzibar, lakini baada ya kuikagua aligundua kuwa lina matatizo na kuamua kulirudisha na kuagiza kitu kipyaaaaaa.

AY ft Marco Chali - Party Zone [Official Video]