Dogo Janja
ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi na kusisitiza kwamba japo
aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile
zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho
amekikubali kwa roho safi.
Janja amesema bado hajasaini
mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu wake wawili anaowasubiri
kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba, baada ya hapo ndio
atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza.
Amesema amebadili mawazo na
sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri ambayo aliahidiwa na Ostaz
Juma meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa shule na kurudishwa
nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni kusoma kwenye shule binafsi nzuri
na pia swala lake la muziki kuzingatiwa.
kwenye
sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na
kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati”
Kwa kumalizia Janja amesema
kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli mbiu ya wakati nilivyokujaga
nilisema nawakalisha matembo sasa hivi nawalaza chali matembo”

